Palestina imekuwa mwanachama kamili wa UNESCO | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.11.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Palestina imekuwa mwanachama kamili wa UNESCO

Mamlaka ya Palestina jana imepata ushindi mkubwa wa kihistoria baada ya UNESCO kuitunuku uwanachama kamili wa shirika hilo.

default

Wajumbe wa UNESCO

Hatua hiyo iliungwa mkono na theluthi mbili ya wanachama wa shirika hilo la elimu na utamaduni la umoja wa mataifa. Hata hivyo ilikosolewa vikali na Israel na mshirika wake wa karibu Marekani. Ikulu ya Marekani ilisema hatua hiyo inadhohofisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israel na Palestina. Na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Marekani Victoria Nuland amesema Marekani inatarajia kusitisha mchango wake kwa shirika hilo unaonzia kiasi cha dola milioni 60 kwa mwezi huu. Rais wa Palestina aliomba nafasi ya kuwa mwanachama kamili wa UNESCO Septemba mwaka huu.

 • Tarehe 01.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/132dU
 • Tarehe 01.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/132dU

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com