Leo Wapakistani wanasherehekea miaka 60 ya nchi yao kujipatia uhuru kutoka kwa Uingereza. Kabla ya hapo, Pakistan ilikuwa sehemu ya India ambayo itaadhimisha uhuru wake hapo kesho, Agosti 15. Kwenye sherehe mjini Islamabad, waziri mkuu Shaukat Aziz, alionya dhidi ya nchi za kigeni kujiingiza katika mambo ya Pakistan.