OUGADOUGOU: Maafikiano yafungua njia kuitisha uchaguzi mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

OUGADOUGOU: Maafikiano yafungua njia kuitisha uchaguzi mpya

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na kiongozi wa chama kikuu cha waasi Guillaume Soro wametia saini maafikiano yanayofungua njia ya kufanywa uchaguzi mpya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Kuambatana na makubaliano hayo,serikali mpya itaundwa na ule mpaka unaozuia mapigano kati ya pande mbili na unaolindwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa na Ufaransa utaondolewa pole pole. Ivory Coast,imegawika sehemu mbili tangu jaribio la kutaka kumpindua Rais Gbagbo mwaka 2002 kutofanikiwa.Eneo la kusini linaongozwa na serikali wakati sehemu ya kaskazini hudhibitiwa na waasi.Kufuatia makubaliano yaliotiwa saini siku ya Jumapili,serikali ya Ufaransa imesema, huenda ikaondosha vikosi vyake kutoka Ivory Coast hivi karibuni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com