Ouattara aapishwa rais wa Cote d´Ivoire
7 Mei 2011Matangazo
Ouattara, anaetambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika nchini humo, hatimaye ameapishwa katika sherehe iliyofanywa katika makao ya rais mjini Abidjan, mji mkuu wa Cote d'Ivoire.
Wakati huohuo maafisa wamesema, rais wa zamani Laurent Gbagbo anatarajiwa kuhojiwa na mwendesha mashtaka wa serikali, katika mji wa kaskazini Korhogo, alikowekwa katika kifungo cha nyumbani.
Mapema wiki hii, Luis Moreno-Ocampo, mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, alisema kuwa ataomba idhini ya kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Cote d'Ivoire.