OUAGADOUGOU : Makubaliano ya Ivory Coast kusainia leo | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

OUAGADOUGOU : Makubaliano ya Ivory Coast kusainia leo

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na kiongozi wa waasi Guilllaume Soro leo hii watatia saini makubaliano yenye lengo la kukomesha mfarakano wa wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Makubaliano hayo yalifikiwa hapo jana na Desire Tagro msaidizi wa Gbagbo na mmojawapo wa viongozi wa kundi la Soro New Forces Movement Louis Dakorey Tabley mbele ya Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso.

Hayo ni matokeo ya mazungumzo ya moja kwa moja yaliopendekezwa na Gbagbo hapo mwezi wa Desemba kuanzisha upya mchakato wa amani katika nchi hiyo iliogawika ya Afrika Magharibi .

Kwa mujibu wa Compaore ambaye anasimamia usuluhishi huo makubaliano hayo ambayo ufafanuzi kamili utatolewa leo hii yanajumuisha utatuzi wa moja kwa moja na wa vitendo kwa matatizo yanayoisibu Ivory Coast.

Compaore hususan ametaja mizozo juu ya kusalimisha silaha za wapiganaji waasi,orodha ya daftari la wapiga kura na maandalizi ya uchaguzi ambao umekuwa ukiendelea kuahirishwa kwa miaka mingi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com