Oslo. Tuzo ya Nobel yaenda kwa mwanauchumi. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Oslo. Tuzo ya Nobel yaenda kwa mwanauchumi.

Nishani ya amani ya Nobel mwaka huu imetolewa kwa Muhammad Yunus na benki yake ya Grameen, mfumo wa benki ya wananchi wa hali ya chini ambao umesaidia mamilioni ya watu nchini Bangladesh.

Watoaji wa tuzo hiyo nchini Sweden wamemsifu Yunus mwenye umri wa miaka 66 pamoja na benki ya Grameen , sio tu kwa mafanikio ya kiuchumi walioweza kusaidia kujenga , bali pia kwa kuimarisha demokrasia na haki za binadamu.

Benki ya Yunus inawasaidia hususan wanawake, kwa kuwawezesha kuanzisha biashara ndogo ndogo bila ya kuwa na dhamana ya kitu. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameueleza mfumo wa benki ya Grameen kuwa ni mfano bora wa ufanyaji biashara kijamii.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com