Osetia kusini imo katika kitendawili; hakuna mshindi kamili katika mzozo huo. | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Osetia kusini imo katika kitendawili; hakuna mshindi kamili katika mzozo huo.

Kwa muda wa mwaka mmoja uliopita rais wa Georgia Mikhail Saakashvili ameshindwa kulirejesha kwa nguvu jimbo linalotaka kujitenga la Ossetia kusini. Urusi ilizuwia hatua kijeshi.

default

Rais wa Georgia President Mikhail Saakashvili akizungumza na majeruhi wa vita hospitalini alipofanya ziara katika hospitali ya jeshi mjini Gori .

Kwa muda wa mwaka mmoja uliopita rais wa Georgia alitaka kwa nguvu kulirejesha katika himaya yake jimbo linalotaka kujitenga la Osetia kusini. Urusi ilizuwia hatua hiyo kijeshi, lakini pamoja na hayo hakuna mshindi halisi katika mzozo huu.

Rais wa Georgia Michail Saakashvilli sio tu ameshindwa kulirejesha jimbo la Ossetia kusini katika mamlaka ya Georgia kijeshi mwaka mmoja uliopita. Mambo mengi yanalega lega, kwa kuwa tangu wakati huo amepoteza uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa. Nchini Georgia upinzani uliokuwapo hapo kabla dhidi yake pamoja na matokeo ya vita hivyo umeongezeka. Ni kwa njia ya ukakamavu pamoja na sehemu ya mbinu zinazotia shaka ndio Shakashvilli ameweza kuendelea kubaki madarakani mjini Tiblis.

Sera za mambo ya kigeni hazionekani kuwa nzuri pia kwa Saakashvili. Katika mataifa ya Ulaya anaonekana kama mwanasiasa asiyeaminika ama mtu wa kubahatisha tu. Katika ripoti iliyotolewa na umoja wa Ulaya kuhusu uungaji wake mkono vita vya siku tano mbinyo bado haujabadilika. Utawala mpya wa Marekani chini ya rais Barack Obama unaendelea kuiunga mkono Georgia bado kuhusiana na nia yake kuelekea kujiunga na umoja wa mataifa ya Ulaya magharibi, lakini makamu wa rais wa Marekani Joe Biden ameonya muda mfupi wakati wa ziara yake nchini humo kuwa mzozo unaohusu kujitenga kwa majimbo ya Georgia hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kivita.

Uwezekano wa Georgia kujiunga na umoja wa NATO ni suala ambalo bado halijafungwa. Katika nyakati nyingine hata hivyo si suala la umuhimu wa juu.

Na kwa upande huo hata hivyo si ushindi kwa Urusi.

Mwaka mmoja baada ya vita , hata kwa upande wa uongozi wa Urusi wa rais Dmitri Medvedev hakuna ushindi wa kisiasa unaoweza kuonekana. Hata hivyo Urusi imeweza kwa mafanikio kulinda hali iliyopo sasa.

Hatua ya kijeshi hata hivyo haikuweza kumuangusha rais wa Georgia Mikhail Saakashvili, kitu ambacho kilikuwa ndio lengo kuu la utawala wa Urusi. Kinyume chake imekuwa ni malipo kwa Urusi kutokana na matumizi makubwa ya kijeshi, hali ya kutokuaminiana imekuwa ya juu zaidi katika mataifa ya Ulaya kuelekea Urusi ambayo inaonekana kuzidi kupata nguvu kijeshi.

Mbali na hayo hatua ya Urusi kuyatambua majimbo yanayotaka kujitenga ya Ossetia kusini na Abkhazia imezidi kuweka hali kuwa ngumu zaidi.

Hatua hiyo sio tu imesababisha Urusi kutengwa kimataifa, lakini hii si mara ya kwanza kwa Urusi kuifuatilia nchi ambayo hapo kabla ilikuwa moja kati ya majimbo ya zamani ya iliyokuwa Urusi.

Mwandishi Mannteufel, Ingo/ZR/ Sekione Kitojo.

Mhariri Mohammed Abdul-Rahman.

►◄

 • Tarehe 06.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/J4cA
 • Tarehe 06.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/J4cA

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com