Olimpiki 2012: Usain Bolt kuthibitisha ubabe wake | Michezo | DW | 09.08.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Olimpiki 2012: Usain Bolt kuthibitisha ubabe wake

Marekani imeshinda mpambano wake mkali dhidi ya mahasimu wao wakubwa katika riadha Jamaica,kwa kushinda mapambano mengi kati yao.Lakini Usain Bolt amefanikiwa kufuzu katika fainali ya mbio za mita 200.

Jamaica's Usain Bolt celebrates after winning the men's 100m final during the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 5, 2012. REUTERS/David Gray (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS)

Usain Bolt bingwa wa mita 100

Usain Bolt atataka kuthibitisha kuwa yeye ni mbabe wa Olimpiki . Huku hayo yakiarifiwa Kenya inapanga kuwania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki mwaka 2024.

Kwa hayo na mengineyo huyu hapa mwanamichezo wetu Sekione Kitojo.

Bolt anaingia katika fainali ya leo ya mbio za mita 200 akitaka kuwa mtu wa kwanza kushinda mbio za mita 100 na 200 katika mashindano ya olimiki mfululizo.

Mwenda mbio huyo kutoka Jamaica pamoja na mshirika wake katika mazowezi ambaye humtania kwa kumuita "Jitu kali" , Yohan Blake, walishinda bila matatizo mbio zao za mchujo za mita 200 katika nusu fainali , wakati wote wakifika mwanzo katika mstari wa mwisho.Ni rafiki yangu mkubwa na nafikiri itakuwa mbio zinazofurahisha sana, amesema Blake alizungumza na waandishi habari.

Bolt amesema kuwa anashauku kubwa kuingia katika fainali ya pambano hilo analolipenda na atashinda, bila shaka.

Siwezi kusema mimi ni bora hadi pale nitakaposhinda mbio za mita 200, amesema Usain Bolt. Ni kutokana na hili , ambapo nitaweza kutetea mataji yangu yote , kwasababu hii ndio itanifanya mimi kuitwa bingwa wa mabingwa.

Kwingineko katika riadha katika siku ya 13 ya michuano ya Olimpiki , David Rudisha wa Kenya anapigiwa upatu kutoroka na medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 na bingwa wa dunia Christian Taylor na Mmarekani mwenzake Will Claye wanapambana katika kuruka mbali mara tatu.

David Lekuta Rudisha of Kenya celebrates after he won the Men's 800 meters during the ISTAF Athletics Meeting in Berlin, Sunday, Aug. 22, 2010. David Rudisha of Kenya has broken the men's 800-meter world record by running 1 minute, 41.09 seconds. Rudisha powered home to beat the previous record of 1:41.11 set by Wilson Kipketer of Denmark in Cologne, Germany on Aug. 24, 1997. (AP Photo/Markus Schreiber)

David Lekuta Rudisha anawania leo kunyakua medali ya dhahabu katika mbio za mita 800.

Anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za wanawake Barbora Spotokova pia anatupia jicho kunyakua dhahabu katika kutupa mkuki wakati Mmarekani anayeshikilia nae rekodi ya dunia Ashton Eaton anawania medali ya dhahabu katika seti ya michezo kumi anayoshiriki kwa pamoja katika riadha, Decathlon.

Marekani imeongeza mavuno yao ya medali za dhahabu hadi kufikia 34 na kuikaribia China katika kileleni cha mavuno ya medali za dhahabu. China ina medali 36 za dhahabu.

Wakati huo huo mji mkuu wa Nairobi unapanga kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2024 na kuwa mji wa kwanza katika bara la Afrika kuwa mwenyeji. Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga jana akiwa mjini London .

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman