1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama azungumza na Waandishi

Admin.WagnerD15 Novemba 2012

Rais Baraka Obama wa Marekani hakuonesha ishara yoyote ya kufikia muafaka na chama cha Republican juu ya bajeti badala yake amesisitiza kupunguza nakisi kwa kuendelea na mpango wa kuwatoza kodi matajiri.

https://p.dw.com/p/16jaY
U.S. President Barack Obama gestures while addressing his first news conference since his reelection, at the White House in Washington November 14, 2012. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Rais Barack ObamaPicha: Reuters

Hata hivyo rais Obama amesema pendekezo la Republican la kuongeza mapato juu ya taifa hilo linatia moyo. Kwa upande wa chama cha Republican wanaendelea kupinga mpango wa obama wa kuwatoza kodi matajiri kwa kwa hoja ya kwamba mpango huo utakwamisha ustawi wa Marekani.

Obama asisitiza punguzo la kodi

Lakini Obama amesisitiza anataka ule mpango wa kupunguza kodi uliyopo uendelee kwa manufaa ya asilimia 98 ya Wamerakni. Lakini utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwaka huu. Hatua hiyo ya Obama inatarajiwa kupunguza athari za kizungumkuti cha bajeti. Yaani mpango wenye lengo la kupunguza nakisi ambao unaweza pia kusababisha mporomoko wa uchumi wa taifa lake.

Kiongozi huyo alitaka taifa liendelee katika jitihada hiyo kwa kuwa itasaidia katika ukuaji wa uchumi, raia kwa ujumla pamoja na kibiashara. Hata hivyo alisisitiza kwamba makubaliano ya kufikia hatua hiyo hayatahusisha kipengelea cha kuongeza kodi kwa matajiri nchini humo mpango ambao kwa kiasi kikubwa unakataliwa na chama cha Republican.

U.S. President Barack Obama gestures while addressing his first news conference since his reelection, at the White House in Washington November 14, 2012. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
USA Pressekonferenz ObamaPicha: Reuters

Mjadala uko wa uchumi uko wazi

Katika mkutano huo wa kwanza na waandishi wa habari tangu kuchaguliwa kwake tena Novemba 6, rais Obama alisema milango ipo wazi kwa yeyote mwenye mawazo mengine mapya katika kustawisha uchumi wa taifa hilo.

hatua za dharura zilizochukuliwa kutokana na mapatano baina ya republican ambazo zinalengo la kuoungeza bajeti ili kustawisha uchumi. Ikiwa hatua hizo zitatekelezwa zinaipunguzia Marekani dola bilioni 600 kwa mwaka ujao na kusababisha mdororo wa uchumi.

Katika mkutano wake huo Obama amezungumza masula kadhaa mengi kadhaa ikiwa mkakati kwa mwaka ujao katika kukabiliana na hali hiyo lakini hata hivyo alikwepa maswali kuhusu mkuu wa shirika la kijajusi la Marekani aliyejiuzulu hivi karibuni David Petraeus.

Katika suala la uhamiaji ameahidi kuharakisha kile alichokiita changamoto kubwa aliyoshindwa kuitekeleza katika awamu yake ya kwanza ya uongozi "mpango madhubuti katika sheria za uhamiaji. Amesema matarajio yake unakuwepo mswaada na unatuambulisha ili kuweza kufanikisha mchakato wa uwepo wa sheria mpya.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri:Yusuf Saumu