1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ataka mapatano yafikiwe juu ya kuutatua mgogoro wa bajeti

Abdu Said Mtullya26 Julai 2011

Viongozi wa Marekani bado hawajafikia mapatano juu ya mgogoro wa bajeti.

https://p.dw.com/p/123F4
Rais Barack Obama akihutubia mgogoro kuhusu BajetiPicha: AP

Rais Obama ametahadharisha juu ya madhara yasiyoweza kupimika kutokana na mzozo wa bajeti.

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni ,Obama amesema ikiwa nakisi ya nchi itaongezeka, athari zake zitakuwa mbaya kwa uchumi na nafasi za ajira. Rais huyo pia ametanabahisha kuwa huenda kwa mara ya kwanza uwezo wa Marekani wa ,kulipa madeni ukateremshwa .

Obama pia ameutetea msimamo wake juu ya kupandisha kodi kwa wenye vipato vya juu na amevitaka vyama vya Demokratik na Republican vifikie mwafaka utakaoziridhisha pande zote. Kwa muda wa wiki kadhaa sasa wawakilishi wa vyama hivyo wamekuwa wanabishana juu suala la kuiruhusu serikali kukopa zaidi kuvuka kiwango cha sasa. Ikiwa Bunge halitaupitisha uamuzi hadi tarehe 2 mwezi ujao serikali ya Marekani itafilisika.

Katika juhudi za kuisawazisha bajeti chama cha Demokratik cha Rais Obama kinataka, siyo tu kupunguza matumizi, bali pia kupandisha kodi. Chama cha Republican kinayapinga hayo katu katu.

Wakati huo huo Shirika la fedhaa la kimataifa limeitaka serikali ya Marekani iongeze haraka kiwango cha kukopa ili iweze kuepuska kushindwa kuyalipa madeni yake. Lakini pia Shirika hilo pia limeitaka Marekani ilidhibiti deni lake ili kuepusha dunia na madhara makubwa ya kiuchumi

Taasisi hiyo imeyasema hayo katika ripoti yake ya mwaka juu ya Marekani. Imesema katika kipindi cha muda mfupi ujao Marekani itapaswa kuyapunguza matumizi hatua kwa hatua, la sivyo itapoteza imani.