1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ahutubia bunge la Uingereza

26 Mei 2011

Rais Barack Obama wa Marekani amelihakikishia bara la Ulaya kuwa litaendelea kuwa sehemu muhimu katika sera za Marekani za mambo ya kigeni.

https://p.dw.com/p/11OE0
Rais wa Marekani Barack Obama wakati akihutubia bunge la UingerezaPicha: AP

Rais wa Marekani Barack Obama amehutubia wabunge katika bunge la Uingereza wakati wa ziara yake ya kiserikali jana Jumatano. Hotuba yake ilikuwa ni sehemu muhimu ya ziara yake katika mataifa ya Ulaya na ilikuwa na lengo la kulihakikishia bara hilo kuwa litaendelea kuwa sehemu muhimu ya sera zake za mambo ya kigeni.

Obama ameimarisha uhusiano maalum kati ya Marekani na Uingereza, na amesema kuwa hali hiyo itaendelea siku za usoni.

Hapo mapema , alipokuwa pamoja na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika mkutano na waandishi habari, Obama amesema mbinyo dhidi ya serikali ya Libya inayoongozwa na kanali Gaddafi hautakoma. Pia amesema kuwa anaimani kuwa suluhisho la mataifa mawili linaweza kufikiwa baina ya Waisraeli na Wapalestina. Rais huyo wa Marekani atakwenda katika mkutano wa mataifa yenye utajiri mkubwa duniani ya G8 katika mji wa Deauville, nchini Ufaransa leo na baadaye atakwenda nchini Poland mwishoni mwa juma.