NOUKCHOUT:Mauritania wasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NOUKCHOUT:Mauritania wasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi

Wananchi wa Mauritania wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa kwanza wa urais wa kidemokrasia toka nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1960.

Raundi ya pili ya uchaguzi ilifanyika jana, baada ya uchaguzi wa kwanza wiki mbili zilizopiza.

Wagombea wawili waziri wa zamani, Sidi Ould Sheikh Abdellahi na kiongozi wa upinzani Ahmed Ould Daddah wanachuana kuwania nafasi hiyo.

Wote wawili waliwahi kufungwa nchini ya utawala wa kijeshi.Matokeo yanatarajiwa kutangazwa hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com