1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahadi ya Obama ya nishati Afrika yagonga mwamba

Admin.WagnerD23 Julai 2015

Wakati Rais Barack Obama wa Marekani akirejea barani Afrika juma hili, utekelezaji wa ahadi ya mipango yake ya kuhakikisha kuwa bara hilo linakuwa na umeme wa uhakika unaelekea kugonga mwamba.

https://p.dw.com/p/1G3bI
Barak Obama besucht Südafrikas Präsident Jacob Zuma
Rais Barack Obama wa Marekani alipotembelea Afrika KusiniPicha: Reuters

Mkwamo huo umetokana na benki ambayo inapaswa kuidhinisha mikopo kwa makampuni ambayo yanatarajiwa kununua bidhaa zinazozalishwa na Marekani kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo kufungwa kutokana na mkataba wake kumalizika.

Kati ya dola bilioni saba ambazo Rais Barack Obama alitenga kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo barani Afrika , dola bilioni tano zinapaswa kuidhinishwa na benki hiyo iliyofungwa na kati ya fedha hizo tayari dola milioni 132 zilikuwa tayari zimeidhinishwa kabla ya mkataba wa benki hiyo kumalizika ambacho ni kikwazo cha upatikanaji wa fedha zaidi.

Bunge la Marekani kunusuru mpango huo

Ingawa mamlaka ya benki hiyo inakiri kuwa bado ina mabilioni ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, haitawezekana hadi hapo bunge la nchi hiyo litakapoamua kuifufua benki hiyo.

Windrad Windräder Erneuerbare Energien Windpark Südafrika Flash-Galerie
Mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya upepo Afrika KusiniPicha: AP

Hali hii inaonekana kuyanyima nafasi makampuni ya kimarekani na kutoa mwanya kwa makampuni ya kichina, taifa ambalo limekuwa likiwekeza kwa kiwango cha juu sana barani Afrika na makampuni yake yangependelea kupata nafasi hiyo.

Andy Herscowitz ambaye ni mratibu wa mpango wa Marekani wa nishati ya uhakika ya umeme barani Afrika anasema makampuni ya marekani ambayo yana uwezo wa kupata mikopo toka serikalini basi yana nafasi kubwa ya kunufaika na zabuni hiyo.

Ndoto za Obama za maendeleo Afrika zaelekea kutoweka

Kwa Rais Obama , mkwamo wa mpango huo, unaonyesha kufifisha ndoto zake za kulifanya bara la afrika kuwa na nishati ya umeme ya kuaminika.

Miaka miwili baada ya Rais Barack Obama kuzindua mpango huo katika ziara yake nchini Arika ya kusini hadi sasa hakuna megawati yoyote ya umeme ambayo imeongezeka kutokana na utekelezaji wa mpango huo kwa bara la Afrika ambalo linakabiliwa na ukosefu mkubwa wa nishati ya uhakika ya umeme.

Kutokana na dalili zilizoanza kuonekana za kukwama katika moja ya vipaumbele vyake vikuu barani Afrika, Rais Obama atashindwa kuwashawishi viongozi wa Afrika wakamuelewa ya kuwa ameweza kutumia nafasi yake barabara kama Rais wa kwanza mweusi wa Marekani kwa kutoa kipaumbele kwa kuleta maendeleo ya uhakika barani Afrika.

Licha ya kuwa ziara ya wiki hii ya Rais Obama nchini Kenya na baadae Ethiopia itakuwa ni ziara yake yake ya tatu kwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara kama Rais wa Marekani Agenda yake kubwa kidunia imeonekna kuangazia zadi mataifa ya bara la Asia na mataifa ya mashariki ya kati.

Mwandishi: Isaac Gamba
Mhariri.: Daniel Gakuba