1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria inapata hasara kwa wizi wa mafuta

5 Juni 2012

Wakati makampuni ya mafuta ya Nigeria yakiendelea na kazi zao za uchimbaji na usafishaji wa mafuta katika maeneo kadhaa, wizi wa mafuta yasiyosafishwa ni tatizo linalolikosesha taifa hilo mapato mengi.

https://p.dw.com/p/1586h
Mitambo ya mafuta Niger Nigeria
Mitambo ya mafuta Niger NigeriaPicha: picture-alliance/dpa

"Eneo hili jirani na Reli wanafanya wizi huo, na hawa ni waharifu waliojipanga vizuri si mwizi mmoja mmoja tu, wanajifarisha kwa kutumia treni wao na mizigo yao, wananunua vifaa vya kubebea mafuta hayo." Anasema mfanyakazi wa Kampuni ya mafuta ya Shell.

Huyo ni miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya kampuni ya Shell ambaye kampuni yake ni miongoni mwa yale yenye mabomba kadhaa ya mafuta yasiosafishwa yanayoibwa kutoka mabomba ya mafuta. Mabomba hayo yanapita kandoni mwa ya reli.

Nigeria Bodo
Nigeria BodoPicha: AP

mmoja wa vijana wanaofanya wizi wa mafuta hayo yasiosafishwa anasema kuwa wakiyaweka mafuta kwenye vyombo maalumu wanayachemsha na kupata Mafuta ya Petroli baadae mafuta ya taa na tena mafuta ya dizeli.

Japokuwa kumekuwepo na askari zaidi ya 26,000 bado wizi huo umekuwa ukiwaumiza vichwa makampuni ya mafuta na kuyasaababishia hasara kubwa. Ambapo takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya mapipa 150,000 yanaibiwa kila siku.

Sambamba na hilo Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala anasema kuwa asilimia 20 ya mapato ya taifa lao inapotea kwa wizi wa mafuta tu ambapo fedha hizo zingekuwa na manufaaa makubwa kwa taifa hilo.

Hali hii inaifanya Serikali ya Rais Goodluck Jonathan aliyetimiza mwaka mmoja sasa akiwa madarakani tangu aingie madarakani kwa mhula wa pili kukabiliwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na tatizo hili.

Katika eneo moja ambapo kazi hiyo ya kusafisha na kunyonya mafuta yasiosafishwa kutoka katika mabomba hayo ilionekana kushamiri kulionekana miti ya mianzi iliyobadilika rangi na kuwa mieusi tii kwa kazi hiyo ya kufyonza mafuta hayo kabla ya kuyapasha moto na kuyasafisha kwa matumizi.

Maeneo yanayofikwa na tatizo hilo ni pamoja na Niger delta ambapo ni nyumbani kwa Rais Jonathan hasa huko Bayelsa ambako madhari yake inapambwa na moshi wa moto unaofuka mitaani kwa kazi hiyo haramu ya wizi wa mafuta.

Mwaka 2009 seriklai ya Nigeria iliamua kuanza kuwalipa kiasi cha Naira 65,000 kwa askari wanaofanya ulinzi katika maeneo hayo angalau kupunguza hali hiyo ya wizi wa mafuta kwani wakati mwingine vijana wanaojihusisha na wizi huoh utumia hongo kuwapa askari hao walinzi.

Mpaka sasa vijana10,000 wameingizwa katika mafunzo maalumu ya ulinzi huo lakini wanafanya kazi katika malalamiko ya kulipwa mishahara midogo,huku makamanda wao wakipokea mishahara mikubwa mno.

Kumekuwa na hadaa lukuki katika eneo hili lenye mafuta tele kama vile elimu, ajira, barabara, shule na hospitalia bora lakin yote hayo imekuwa kama ni danganya toto tu kwa wananchi hao ambapo ardhi yao ina utajiri mkubwa.Mafanyakazi huyu anasema.

Nigeria Ogoniland
Nigeria OgonilandPicha: AP

" Kuna watu wanatafuta utajiri kwa kuharibu mazingira ambayo ni kwa vizazi vyetu vijavyo ninakuwa na huzuni sana." alisema mfanyakazi huyo wa kampuni ya mafuta ya Shell.

Hali hiyo aliyoisema mfanyakazi wa kampuni ya shell inaungwa mkono na shirika la Umoja wa Matiafa la Mpango wa Mazingira (UNEP) likisema kuwa hali hii itaigharimu Nigeria muda wa miaka 30 na dola bilioni moja kuweza kukamilisha mpango wake wa kuondoa uchafuzi wa mazingira katika eneo la Delta.

Mwandishi:Adeladius Makwega/RTRE.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

.