Niebel kutembelea leo Dadaab Kenya
16 Agosti 2011Matangazo
Leo waziri wa ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel atakwenda Dadaab, kabla ya kuwa na mkutano na waandishi habari mjini Nairobi baadae jioni.
Jana waziri Niebel alifanya mazungumzo na Rais Mwai Kibaki, mawaziri wengine wa ngazi ya juu wa serikali ya Kenya, wawakilishi wa Umoja wa Afrika na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na wakimbizi, UNHCR.