1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NIAMEY.Chad kuwatimua raia kutoka nchi jirani

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzI

Serikali ya Niger imesema kuwa itawafukuza kutoka nchini humo raia laki moja na elfu hamsini wa kiarabu walioingia nchini humo miaka 20 iliyopita kutoka nchi jirani ya Chad.

Waziri wa mambo ya ndani wa Niger amesema hatua hiyo inafuatia kuzidi hali ya mvutano kati ya wageni hao na raia wa Niger katika eneo la mpakani la Diffa.

Warabu kutoka nchi jirani ya Chad walikimbilia nchini Niger katika mika ya 80 baada ya kuzuka mapigano nchini mwao.

Chad ilikabiliwa na vita wakati huo ambapo majeshi yaliyoungwa mkono na Libya yalipojaribu kuitwaa nchi hiyo.