Ni msimamo wa pamoja | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ni msimamo wa pamoja

Mkutano wa dharura wa nchi zinazoitumia sarafu ya euro unafanyika hii leo,huku Ujerumani na Ufaransa zikifikia msimamo wa pamoja kuhusu kuipa mkopo wa pili Ugiriki

default

Rais wa Ufaransa Nicolas Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, wamekubaliana kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo wa madeni wa Ugiriki, huku mkutano wa dharura wa eneo linaloitumia sarafu ya euro ukitarajiwa kufanyika hii leo.

Symbolbild Grafik Eurokrise Europa Euro Währungskrise

Msemaji wa Merkel alikataa kufichuwa yaliyomo kwenye mpango huo, lakini alisema kuwa viongozi hao wawili walifikia mtazamo wa pamoja kuhusu mzozo huo wa madeni pamoja na benki kuu ya Ulaya na rais wa Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy mapema hii leo, baada ya mazungumzo ya jana usiku.

Ugiriki inahitaji kiasi ya euro bilioni 110 zaidi, kuimarisha fedha zake hadi mwishoni mwa mwaka 2014. Rais wa baraza la Umoja huo, Jose Manuel Barroso, amesema ni lazima suluhu ya uhakika ipatikane hii leo, la sivyo alionya kuwa uchumi duniani utaathirika.

Symbolbild Krise Euro EU Währung Schulden

Masoko yana wasiwasi kuwa Ugiriki ikishindwa kulipa madeni yake, itazusha athari katika nchi nyengine zinazoitumia sarafu hiyo ya euro, ambayo itaziathiri pia nchi zenye uchumi thabiti Ulaya.

Mwandishi:Maryam.Abdalla/ afp, reuters, dpa
Mhariri:Yusuf, Saumu

 • Tarehe 21.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/120fD
 • Tarehe 21.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/120fD

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com