NEW YORK:Zimbabwe yakataa kuingiliwa kati | Habari za Ulimwengu | DW | 28.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Zimbabwe yakataa kuingiliwa kati

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amezitaka Uingereza na Marekani kutojiingiza kwenye mambo ya ndani ya nchi yake.

Rais Bush alizungumzia juu ya mateso yanayowakabili raia wa kawaida nchini Zimbabwe chini ya utawala dhalimu wa Zimbabwe.

Akizungumza kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa rais Mugabe nae hasa amemshambulia rais George Bush wa Marekani.

Kwa kusema kuwa mikono ya kiongozi huyo inachuruzika damu ya raia wasio na hatia huko Irak na Afghanistan huku ikitakiwa atambuliwe kuwa ni kinara wa kutetea haki za binadamu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com