NEW YORK:UN yarefusha muda wa vikosi vyake Ivory Coast | Habari za Ulimwengu | DW | 17.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:UN yarefusha muda wa vikosi vyake Ivory Coast

Umoja wa Mataifa umepiga kura kurefusha muda wa majeshi ya kulinda amani ya umoja huo na yale ya Ufaransa kuendelea kuwepo nchini Ivory Coast mpaka mwakani.

Hatua hiyo ni katika kusaidia kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Rais Laurent Gbagbo ameahidi kufanyika kwa uchaguzi huo tarehe 31 mwezi Desemba, baada ya kucheleweshwa na kuahirishwa mara kadhaa.

Ivory Coast imegawanyika katika pande mbili toka waasi walipotwaa eneo la kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002—2003.

Mpango wa kuiunganisha tena nchi hiyo ulianza mwezi March mwaka huu, pale kiongozi wa waasi Gulliano Soro alipoteuliwa kuwa waziri mkuu.Hata hivyo mpango huo uko katika hatari, kufuatia jaribio la kutaka kumua waziri mkuu huyo, pale ndege yake iliposhambuliwa kwa kombora mwezi uliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com