NEW YORK:Kansela Merkel ahimiza juhudi za kupambana na ongezeko la joto
25 Septemba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel ametoa mwito juu ya kupambana na ongezeko la joto duniani. Akizungumza mjini New York kwenye mkutano uliodhaminiwa na Umoja wa Mataifa juu ya suala la hali ya hewa Kansela Merkel amezitaka nchi za viwanda ziwe mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.