NEW YORK:Cuba yasema Bush aliingia madarakni kwa wizi wa kura | Habari za Ulimwengu | DW | 27.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Cuba yasema Bush aliingia madarakni kwa wizi wa kura

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Felipe Perez Roque amesema kuwa Rais George Bush wa Marekani aliingia madarakani kwa ghila na wizi wa kura kwahiyo hana mamlaka au uwezo wa kumuhukumu mtu yoyote.

Katika hutoba yake kwenye mkutano wa ngazi ya mawaziri katika Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa, waziri huyo wa nje wa Cuba pia alimshutumu Rais Bush kwa kuruhusu wafungwa kuteswa katika gereza la kijeshi la Guantanamo Bay.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alimuunga mkono waziri huyo wa nje wa Cuba kwa kusema kuwa nchi yake imekuwa adui wa Marekani na Uingereza baada ya kukataa tabia yao ya kutaka kutawala.

Naye kiongozi wa mrengo wa kushoto wa Bolivia Evo Morales alitupilia mbali tuhuma za Rais Bush dhidi ya utawala wa Fidel Castro akisema kuwa Castro ametuma majeshi katika nchi nyingine kuokoa maisha ya watu, lakini Bush anatuma majeshi kwenda kusambaratisha maisha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com