1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wito wa kupeleka vikosi vya amani Somalia

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVT

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa Umoja wa Afrika kupeleka vikosi vyake vya amani nchini Somalia kama ilivyokubaliwa,ili kuzuia pengo la usalama.Baadae vikosi vya Ethiopia vilivyoisaidia serikali ya mpito ya Somalia Desemba mwaka jana,kuwatimua wanamgambo wa Kiislamu,vitaweza kurejea nyumbani.Umoja wa Afrika hivi karibuni katika mkutano wake wa kilele,ulikubali kimsingi kupeleka wanajeshi 8,000 kulinda amani nchini Somalia.Hadi hivi sasa,ni nchi tatu tu zilizokubali kushiriki na kupeleka kama wanajeshi 4,000.Juma lijalo,wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watakutana kushauriana njia ya kuutenzua mgogoro huo.