NEW YORK .watoto wa Chad siyo yatima | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK .watoto wa Chad siyo yatima

Idadi kubwa ya watoto 103 waliokusudiwa kutolewa nje ya Chad na shirika la hisani la Ufaransa wana familia zao.

Taarifa ya pamoja ya asasi 2 za Umoja wa Mataifa na chama cha msalaba mwekundu duniani imesema hayo, na kueleza kuwa haiwezekani kuwatia watoto hao katika fungu la yatima.

Ripoti hiyo imesema watoto hao wana jamaa wa karibu angalau mmoja anaewalea.

Ripoti hiyo pia imesema,watoto hao ni raia wa Chad na hawatoki jimbo la Darfur kama ilivyodaiwa na shirika la Ufaransa hapo awali.

Raia tisa wa Ufaransa,saba wa Uhispania na wawili wa Chad walikamatwa wiki jana walipokuwa wanafanya matayarisho ya kuwasafirisha watoto hao ili kuwapeleka Ulaya.

Watu hao sasa wanakabiliwa na mashtaka ya jaribio la kuwateka nyara watoto hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com