New York. Uingereza yataka Sudan kuwekewa vikwazo. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Uingereza yataka Sudan kuwekewa vikwazo.

Balozi wa Uingereza katika umoja wa mataifa , Emyr Johns parry ametishia kuwekewa vikwazo Sudan baada ya rais Omar al-Bashir kutoa masharti kadha kuhusiana na uwekaji wa majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Jones Parry amesema azimio kuhusu vikwazo hivyo linaweza kutolewa hadi wiki ijayo na inaweza kuwa pamoja na kuzuwia ndege za Sudan kuruka katika eneo la Darfur na kupanua marufuku ya kutosafiri pamoja na kuzuwia mali za nchi hiyo.

Kikosi cha pamoja cha majeshi ya Umoja wa Afrika na umoja wa mataifa chenye wanajeshi wapatao 20,000 kinatarajiwa kupelekwa huko Darfur.

Hapo mapema Sudan ilikataa ripoti ya ujumbe wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa ambayo inaishutumu Sudan kwa kuchochea na kushiriki katika kuendea kinyume haki za binadamu pamoja na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Kwa mujibu wa makadirio ya umoja wa mataifa, kiasi cha watu 200,000 wameuwawa na zaidi ya milioni 2.5 wamekimbia makaazi yao tangu mzozo huo ulipoanza miaka minne iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com