NEW YORK :Uamuzi wa mauaji ya Kilwa watatanisha | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK :Uamuzi wa mauaji ya Kilwa watatanisha

Kiongozi wa Kamisheni ya Umoja wa mataifa ya Haki za Binadamu UNHCR anaeleza wasiwasi wake kufuatia uamuzi wa mahakama ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wa kuachia wahusika wa mauaji ya Kilwa.

Bi Louise Arbor kiongozi wa Kamisheni hiyo anatoa wito kwa uongozi nchini Kongo kutumia njia zote zile za kisheria ili kuhakikisha kuwa haki inatimizwa kwa waliopoteza maisha yao katika mauaji ya Kilwa.

Wanachama wa kundi la FARDC waliokoa mji wa Kilwa uliotekwa na waasi kwa muda mfupi mwaka 2004.Uchunguzi uliofanywa na maafisa wa kutetea haki za binadamu wa jumbe wa Umoja wa mataifa wa MONUC nchini Kongo ulibaini kuwa vitendo vya mateso,kuzuiliwa kinyume na sheria na wizi vilitokea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com