NEW YORK: Syria yalalamika rasmi kwa baraza la usalama kuhusu Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 12.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Syria yalalamika rasmi kwa baraza la usalama kuhusu Israel

Syria imewasilisha lalamiko rasmi kwa Umoja wa Mataifa juu ya hatua ya ndege za Israel kuingia katika anga yake kinyume cha sheria wiki iliyopita na kuangusha silaha.

Mjumbe wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar Jaafari amesema serikali yake inataka ulimwengu ufahamu juu ya hatua ya Israel kuihujumu Syria kinyume cha sheria uza kimataifa.

Katika barua yake kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na balozi wa Ufaransa Jean-Maurice Ripert, rais wa sasa wa baraza la usalama, Bashar Jaafari, amesema ndege za Israel zilivuka mpaka na kuingia eneo la kaskazini mwa Syria Alhamisi iliyopita na kuangusha mabomu ambayo hayakusababisha uharibifu wa mali wala majeruhi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com