1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Njama ya kuripua uwanja wa ndege wa JFK

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvJ

Polisi mjini New York wamesema,wamezuia njama ya kundi linalotuhumiwa kuwa ni la kigaidi.Wamesema, wanamgambo hao walipanga kushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F.Kennedy katika jiji la New York na kuripua matangi na mabomba ya mafuta ya ndege.Watu 3 wamekamatwa:mmoja mini New York na wengine 2 nchini Trinidad.Mshukiwa wa nne yuko mbioni.Kwa mujibu wa polisi,mtuhumiwa mmoja aliekamatwa alifanya kazi katika idara ya mizigo kwenye uwanja wa ndege wa JFK na ni raia wa Marekani mwenye asili ya Guyana.Inasemekana kuwa mchongezi wa polisi alirekodi mpango wa mshukiwa huyo.Kwa mujibu wa polisi,mtuhumiwa mwengine ambae hapo zamani alikuwa mbunge wa Guyana, alikamatwa Trinidad siku ya Ijumaa,alipokuwa akijaribu kukimbilia Venezuela.Msemaji wa Idara ya Upelelezi ya Marekani,FBI amesema,njama hiyo imeweza kuzuiliwa mapema.Polisi imesema,mabomba ya mafuta yanayosafirisha mafuta hadi uwanja wa ndege wa JFK hupitia maeneo ya wakazi.