1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama laitaka Iran iwaachie wanamaji wa Uingereza

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCE7

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana juu ya taarifa ya pamoja inayoelezea wasiwasi mkubwa juu ya kukamatwa kwa wanajeshi 15 wa Uingereza na Iran.

Taarifa hiyo pia inaitaka Iran iwaachilie huru wanajeshi hao mara moja.

Mwenyekiti wa sasa wa baraza la usalama ambaye pia ni balozi wa Afrika Kusini katika Umoja wa Mataifa, Dumisani Kumalo, aliisoma taarifa hiyo iliyoandaliwa baada ya saa kadhaa za majadiliano.

Taarifa hiyo ni mfano wa ile iliyotolewa na Uingereza ikilaani hatua za serikali ya Tehran lakini ikapunguza ukali wa maneno yaliyotumiwa na Uingereza.

Urusi imeipinga taarifa hiyo.