1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban kuupa kipaumbele mzozo wa Darfur

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezipa kipaumbele juhudi za kuumaliza mzozo wa kibinadamu wa Darfur nchini Sudan.

Katika siku yake ya kwanza kazini mjini New York hapo jana, Ban alitangaza anataka kushiriki katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu mjini Addis Ababa Ethiopia. Anataka pia kuzungumza na rais wa Sudan, Omar el Bashir katika mkutano huo.

Sudan haijabanduka kutoka kwa msimamo wake wa kupinga kupelekwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kulinda amani Darfur.