NEW YORK: Ban Ki Moon aitetea Libya | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ban Ki Moon aitetea Libya

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameitetea Libya kama nchi kutakakofanyika mazungumzo muhimu kuhusu mzozo wa Darfur licha ya ripoti mbaya za ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Ban Ki Moon kwa kushauriana na serikali ya Sudan, wiki iliyopita alitangaza mkutano kati ya serikali ya Sudan na waasi wa Darfur ufanyike tarehe 27 mwezi Oktoba mwaka huu mjini Tripoli Libya. Lengo la mkutano huo ni kuziongezea nguvu juhudi za kutafauta amani kabla kikosi cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 26,000 wa kulinda amani kupelekwa Darfur.

Ban Ki Moon amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kwamba atafanya mkutano kuhusu Darfur mnamo tarehe 21 mwezi huu kabla kufanyika mkutano wa mjini Triploli Libya.

Katibu mkuu huyo amesema Libya imechaguliwa kwa kuwa imekuwa na jukumu muhimu la upatanishi tangu mwaka jana ikiwa ni pamoja na kuandaa mikutano iliyofanyika mwezi wa Aprili na Julai.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com