NEW YORK: Ban atoa wito kuidhinisha vikosi vya amani | Habari za Ulimwengu | DW | 17.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ban atoa wito kuidhinisha vikosi vya amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon amelishauri Baraza la Usalama,kutoa idhini ya kupeleka vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ban amewasilisha pendekezo la kutuma vikosi vya kimataifa kwenye mipaka ya nchi hizo mbili kwa azma ya kulinda maelfu ya wakaazi wanaokabiliwa na vitisho vya mgogoro wa Darfur katika nchi jirani Sudan.Vile vile kuna zaidi ya wakimbizi 250,000 kutoka Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com