1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban atoa mwito kutafuta suluhisho

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu mapigano,kati ya vikosi vya serikali na wanajeshi waasi,mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wakati huo huo ametoa mwito kwa pande zote mbili kutafuta suluhisho la amani.Wanajeshi waasi wanaongozwa na Jemadari wa zamani Laurent Nkunda.Kwa mujibu wa UNHCR-hadi watu 170,000 mwaka huu wamekimbia eneo la mapigano.kimbia