1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Azimio dhidi ya Iran kupigiwa kura leo

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCh4

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa leo hii linapanga kupiga kura juu ya azmio lenye kuiwekea vikwazo mpango wa nuklea wa serikali ya Iran lakini Urusi bado haikusaini kuchukuliwa kwa hatua hiyo.

Baada ya Uingereza,Ufaransa na Ujerumani kufanyia marekebisho fulani rasimu ya azimio hilo hapo jana Balozi wa Ufaransa Jean-Marc de Sabliere amewaambia waandishi wa habari kwamba wanakutana leo hii kwa ajili ya kulipigia kura azimio hilo.

Kwa mujibu wa wanadiplomasia walio karibu na mazungumzo hayo Urusi haitazamiwi kupata maelekezo ya mwisho hadi hapo Rais Valdimir Putin atakapokutana na washauri wake wa usalama mapema leo hii.

Azimio hilo linaitaka serikali ya Iran ikomeshe shughuli zote za kurutubisha uranium ambazo zinaweza kuzalisha nishati kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea pamoja na mabomu na kusitisha utafiti na utengenezaji ambao unaweza kutengeneza au kupelekea uundaji wa silaha za nuklea.