1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Athari za janga la kinyukliya la Chernobyl ni kubwa mno.

18 Aprili 2006
https://p.dw.com/p/CBJ0

Jumuiya ya kuhifadhi mazingira ya Greenpeace imedai kwamba athari kwa afya kutokana na balaa la kinyuklia lililotokea Chernobyl huko Ukraine miaka 20 iliopita ilidharauliwa sana. Katika ripoti mpya iliotolewa leo, jumuiya hiyo ilisema tarakimu rasmi za Umoja wa Mataifa zinazokisia vifo 4,000 vya ugonjwa wa saratani kufuatana na miyale ya kinyukliya ni za chini mno. Makadirio ya Jumuiya ya Greenpeace ni kwamba kunaweza kuweko vifo zaidi ya laki moja vya ugonjwa wa Saratani, vingi vikitokea Ukraine, Belarusia na Russia. Mripuko na moto uliotokea katika kinu cha kinyukliya cha Chernobyl hapo April mwaka 1986 hadi sasa ni ajali mbaya kabisa ya kinyukliya iliowahi kutokea. Ilitoa vumbi la miyale iliosamabaa kaskazini na magharibi ya Ulaya na mbali hadi Mashariki ya Marekani.