1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Ahmedinejad kuhutubia Baraza la Usalama

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina kipingamizi kwa ombi kutoka kwa Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran kuhutubia nchi wanachama wa baraza hilo kabla ya kupiga kwa azimio la kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa kugoma kusitisha mpango wake wa nuklea.

Balozi Dumisani Kumalo wa Afrika Kusini ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama amesema baraza hilo limekubali ombi la Rais Ahmedinejad kutetea mpango wake wa nuklea katika kikao cha baraza hilo hapo wiki ijayo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean McCormark amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali ya Marekani inataka kumpa viza Ahmedinejad baada ya rais huyo wa Iran kuomba viza kadhaa za kuingia Marekani kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hakuna tarehe iliopangwa ya kupigia kura azimio la vikwazo kadhaa vipya walivyokubaliana nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani baada ya mazungumzo ya zaidi ya wiki mbili.