1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI. Viongozi wahimiza ushiríkiano katika vita dhidi ya ugaidi

4 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCd

Viongozi kutoka nchi za kusini mwa Asia wanaokutana mjini New Delhi wametoa mwito wa kushirikiana pamoja katika vita dhidi ya ugaidi katika eneo hilo.

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo waziri mkuu wa India Manmohan Singh amesema eneo la kusini mwa Asia linahaitaji kuwa na usalama ili kupiga hatua za kimaendeleo.

Nchi hizo zilianzisha umoja wa nchi za kusini mwa Asia mwaka 1985 kwa lengo la kukuza uchumi wake kwa kufanya biashara huru miongoni mwa nchi wanachama lakini bado lengo hilo halijatimia kutokana na ushindani kati ya India na Pakistan.

Wanachama wa nchi za umoja wa kusini mwa Asia ni pamoja na Bangladesh, Nepal, Sri Lanka visiwa vya Maldives na Bhutan.

Afgfhanistan inashiriki katika mkutano huo kwa mara ya kwanza.