1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Utulivu nchini Afghanistan muhimu kwa usalama duniani

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrK

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan ameonya kuwa ukosefu wa utulivu nchini Afghanistan unahatarisha eneo hilo zima.Alipozungumza New Delhi nchini India kwenye mkutano kuhusika na uchumi na ujenzi mpya wa Afghanistan,Karzai alisema,ugaidi na makundi ya wanamgambo yanahatarisha eneo zima na ameomba msaada wa kimataifa kupambana na Wataliban wanaoibuka upya nchini Afghanistan.Waziri mkuu wa India Manmohan Singh akikariri wasi wasi wa Karzai,alisema amani nchini Afghanistan ni muhimu kwa usalama wa kanda hiyo na ulimwengu mzima kwa jumla.Wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo wa kilele wa siku mbili mjini New Delhi.Wajumbe hao ni kutoka nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda G-8,mashirika ya fedha ya kimataifa na taasisi za Umoja wa Mataifa.