NEW DELHI: Msimu wa masika wasababisha mafuriko India | Habari za Ulimwengu | DW | 23.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI: Msimu wa masika wasababisha mafuriko India

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini India yameua si chini ya watu 39.Katika jimbo la kusini la Andhra Pradesh,hadi watu 35 walifariki katika mafuriko ya ghafula katika kipindi cha saa 24.Si chini ya wakazi 200,000 wamehamishwa maeneo mengine.Vile vile watu 4 walifariki katika jimbo la Kerala.Msimu wa masika umesababisha hasara kubwa na umevuruga usafiri wa matreni na magari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com