1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI: Mripuko wa bomu sokoni umeua watu 4

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpF

Si chini ya watu 4 wameuawa na hadi 35 wengine wamejeruhiwa baada ya bomu kuripuka katika soko lililojaa watu,kaskazini-mashariki ya India. Shambulizi hilo limetokea katika mji wa Guwahati, kwenye jimbo la machafuko la Assam.Bomu lilifichwa kwenye baiskeli iliyoegezwa mbele ya msikiti ulio karibu na soko.Mripuko huo ulitokea saa chache kabla ya Michezo ya Riadha ya Asia ya Grand Prix kufunguliwa katika mji wa Guwahati. Michezo hiyo inahudhuriwa na zaidi ya wanariadha 200 kutoka nchi 20.