1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI : Mafuriko yaathiri mamilioni Asia Kusini

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBc4

Zaidi ya watu milioni 35 wameathiriwa na mafuriko makubwa ya pepo za msimu za mvua za masika kusini mwa bara la Asia.

Takriban watu milioni 10 hawana mahala pa kuishi au mawasiliano na vijiji vyao yamekatika, wakiwa na nafasi ndogo au kukosa kabisa chakula na huduma za afya.Kuna uhaba wa maji safi ya kunywa na watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayoletwa na mafuriko kama vile kuharisha,homa ya matumbo na kipindupindu.

India ya Kaskazini,Bangladesh na Nepal ndizo zilizoathirika zaidi.Makadirio ya jumla ya vifo yanatofautiana sana kuanzia mamia kadhaa hadi kupindukia 1,000.

Makundi ya misaada yametowa wito wa michango huku kukiwepo na onyo la uhaba wa chakula na madawa.