1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Negroponte Pakistan

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlx

ISLAMABAD:

Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani John Negroponte akiwa nchini Pakistan, amemtaka rais wa Pakistan,Jamadari Musharraf kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa,kuondoa vizuwizi alivyoviwekea vyombo vya habari nchini,kuifuta hali ya hatari na kuhakikisha uchaguzi huru na bila mizengwe Januari,mwakani.

Waziri huyo wa Marekani alizungumza pia kwa simu na kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto.

Hadi sasa , jamadari musharraf amekataa kuiondoa hali ya hatari aliotangaza akidai itaondoshwa tu pale hali ya usalama itakapotengenea.

Serikali yake imejaribu kuvifunga vituo 2 vikuu vya TV vya kibinafsi-GEO na ARYONE vilivyokuwa vikitangaza kutoka Dubai. Waandishi habari wa pakistan wamelalam ika juu ya ukaguzi wa habari kwa kuandamana katika mji wa Karachi.

Kutoka Washington,kuna taarifa kwamba Marekani inazingatia kumuacha mkono jamadari Musharraf.