1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N'DJAMENA:Watuhumiwa wa njama ya utekaji wanyimwa dhamana

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1P

Umati wa kundi la vijana wameandamana kwenye barabara za mji mkuu wa Chad wa N’Djamena ili kupinga jaribio la njama ya kuwateka watoto zaidi ya 100 wa Kiafrika na kuwasafirisha hadi mataifa ya Ulaya.Yapata vijana 100 walikusanyika katikati ya mji wa N’Djamena ili kuadhimisha uhuru wa taifa hilo kutzoka kwa Ufaransa ndipo walipoanza maandamano hayo.Rais Nikolas Sarkozy wa Ufaransa alizuru nchi ya Chad katika majuma ya hivi karibuni ili kuwezesha raia wake kadhaa walioachiwa kufuatia tuhuma za kuhusika na njama hiyo iliyohusisha shirika la Ufaransa la kutoa misaada kwa watoto Zoes Ark.Wakati huohuo jaji mmoja nchini Chad amewanyima dhamana wafanyikazi sita wa shirika hilo la Zoes Ark na kuamuru kuwa waendelee kuzuiliwa.Raia wengine 3 wa Chad wanaodaiwa kushiriki katika njama hiyo aidha wanazuiliwa.