N’DJAMENA : Watoto 74 waliosafirishwa Ufaransa kuchunguzwa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

N’DJAMENA : Watoto 74 waliosafirishwa Ufaransa kuchunguzwa

Chad itachunguza repoti kwamba takriban watoto 74 wa Chad walisafirishwa kupelekwa Ufaransa zaidi ya mwezi mmoja uliopita bila ya kutaarifiwa wazazi wao.

Mtandao wa makundi ya haki za binaadamu nchini Chad wamewaandikia idara ya waendesha mashtaka wa serikali juu ya watoto hao 74 ambao walisafirishwa kutoka Chad hadi uwanja wa ndege wa kijeshi nje ya Paris hapo tarehe 17 mwezi wa Septemba.

Masngarel Kagali wa idara ya waendesha mashtaka wa serikali amesema haijulikani nani aliehusika na kuwasafirisha watoto hao nje ya Chad lakini yumkini likawa sio kundi la kutowa misaada la Zoe’s Ark la Ufaransa ambalo limezuiliwa kuwasafirisha watoto kutoka Chad wiki iliopita.

Wafanyakazi sita wa Ufaransa wa shirika hilo la Zoe’s Ark wamefunguliwa mashtaka nchini Chad ya kuteka nyara na kutaka kuwasafirisha watoto 103 kwa ndege kuelekea Ufaransa wakidai kuwa ni mayatima kutoka jimbo la Dafur nchini Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com