1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya jeshi la Kenya yaanguka

18 Aprili 2024

Ndege ya kijeshi ya Kenya iliyokuwa imembeba Mkuu wa Majeshi, Francis Ogolla, imeanguka katika mpaka wa Kaben-Cheptule kati ya Elgeyo Marakwet na Kaunti ya Pokot Magharibi.

https://p.dw.com/p/4ewNw
Rais William Ruto wa Kenya.
Rais William Ruto wa Kenya.Picha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Kulingana na chanzo kimoja cha polisi kilichozungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari watano walifariki papo hapo na wengine watatu wamenusurika wakati ndege hiyo ilipoanguka magharibi mwa Kenya mchana wa Alhamisi (Aprili 18).

Soma zaidi: Wafanyabiashara wa Haiti walilia kuchelewa polisi wa Kenya

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji wa serikali ya Kenya, Isaac Mwaura, alihimiza utulivu na kusema kwamba taarifa rasmi kuhusu ajali hiyo ingelitolewa hivi karibuni.