1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Ulaya ziwajibike zaidi Afghanistan

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Katibu mmkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO ahimiza Marekani isiachwe peke yake Afghanistan

https://p.dw.com/p/HM9o

Berlin:


Katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO,Jaap de Hoop Scheffer,ametoa mwito nchi za Ulaya ziwajibike kwa nguvu zaidi nchini Afghanistan. Katibu mkuu Jaap de Hoop Scheffer ametoa mwito huo siku chache tuu kabla ya mkutano wa kilele wa jumuia hiyo mijini Strassburg nchini Ufaransa na Baden Baden nchini Ujerumani.Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani "Bild am Sonntag" katibu mkuu huyo wa jumuia ya kujihami ya NATO, amesema tunamnukuu "kuwaachia wamarekani peke yao haitoshi"-mwisho wa kumnukuu Jaap de Hoop Scheffer aliyesisitiza nchi za Ulaya pia zinastahiki kuwajibika zaidi kijeshi au katika sekta za maendeleo ya jamii."Ujerumani inachangia,"anasema na kutaraji nchi nyengine pia zitafuata mfano huo.Ijumaa iliyopita rais Barack Obama wa Marekani alitangaza mkakati mpya wa nchi yake kwa Afghanistan.Mkakati huo unatilia mkazo umuhimu wa kuizidishwa idadi ya wanajeshi,kuimarishwa ushirikiano wa kimataifa na kupatiwa mafunzo vikosi vya usalama vya Afghanistan.Rais Barack Obama anapanga kuutetea mkakati huo wakati wa mkutano wa kilele wa jumuia ya kujihami ya NATO April tatu na nne ijayo mijini Strassburg na Baden Baden.