1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

NATO yapeleka makaazi ya muda Uturuki

Grace Kabogo
20 Februari 2023

NATO inapeleka makontena 1,000 nchini Uturuki kwa ajili ya kutumika kama makaazi ya muda kwa takribani watu 4,000 baada ya kuathiriwa na matetemeko ya ardhi yaliyolikumba eneo la mpaka wa Uturuki na Syria.

https://p.dw.com/p/4NjnM
Türkei Erdbeben l NATO verschifft Hilfs-Container in die Türkei
Picha: JFC Naples/NATO

Muungano huo wa kijeshi umesema meli ya kwanza iliyopakia makontena 600 imeondoka kwenye bandari ya Italia ya Taran jana jioni.

Makontena hayo yanatarajiwa kuwasili katika mji wa pwani wa Uturuki wa Iskenderun uliopo kwenye jimbo la Hatay wiki ijayo.

Siku ya Alhamisi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg aliizuru Ankara na jimbo lililoathiriwa vibaya kusini mwa Uturuki na kuahidi msaada zaidi.

Takribani nyumba 225,000 zimeathiriwa na matetemeko hayo ya ardhi. Mamlaka ya Majanga ya Uturuki, AFAD, jana usiku ilitangaza idadi ya waliokufa kwa matetemeko hayo imefikia 41,020, na 5,900 wamekufa nchini Syria.