1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

NATO kuondoka Libya 31 Oktoba

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepiga kura kwa pamoja kuunga mkono kumalizika operesheni za vikosi vya kimataifa nchini Libya tarehe 31 mwezi huu Oktoba

default

NATO imesaidia katika operesheni ya miezi 7 Libya kuuondoa utawala wa Muammer Gaddafi

Maafisa wa shirika la kujihami la NATO wanatarajiwa kukutana mjini Brussels Ubelgiji hii leo (28.10.11), kutangaza rasmi mwisho wa operesheni yake ya vita vya angani vya miezi 7 nchini Libya.

NATO Anders Fogh Rasmussen

Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen

Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen hapo jana amesema NATO ipo tayari kuusaidia utawala mpya katika kuingia kwenye demokrasia pekee, lakini hakuna jukumu la ziada kwa shirika hilo nchini Libya, na hii inatoa nafasi ya kumalizika operesheni ya NATO mwishoni mwa mwezi huu.

Mashambulio ya NATO yalichangia pakubwa katika kuondolewa madarakani utawala wa kiongozi wa zamani Muammer Gaddafi.

Hatahivyo utawala wa mpito Libya umeiomba NATO kuendeleza kampeni yake hadi mwishoni mwa mwaka huu ukisema kuwa wafuasi wa Gaddafi bado ni kitisho kwa nchi hiyo.

Mwandishi: Maryam Abdalla/alle

 • Tarehe 28.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/130Wl
 • Tarehe 28.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/130Wl

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com