1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani atakuwa Papa mpya?

Mohamed Abdulrahman13 Machi 2013

Mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani unaendelea wakati huu jopo la makadinali linapokutana rasmi kwa kazi hiyo, huku swali linaloulizwa ikiwa safari hii pia Papa atatoka Ulaya au bara jengine!

https://p.dw.com/p/17up5
Jopo la makardinali wanaokutana kumchagua Papa mpya.
Jopo la makardinali wanaokutana kumchagua Papa mpya.Picha: Getty Images

Wapo makadinali kadhaa ambao watu wameanza kuwafikiria, kama vile Schere kutoka Brazil, Salazar Gomez wa Colombia na Turkson kutoka Ghana. Lakini matakwa ya wengi ni kuwa na Papa kijana. Macho ya wengine yanammulika Kadinali Joachim Meisner kuweza kushika nafasi hiyo kuwa mrithi wa Kadinali Joseph Rätzinger - Papa Benedikti wa 16 .

Suala la Umri

Papa mpya anatakiwa awe mtu mwenye afya nzuri. Meisner ana umri wa miaka 70 na ni mtu imara na msomi kama Rätzinger na msimamo wake ni mchanganyiko wa Wojtyla yaani Papa John Paul wa pili na Rätzinger.

Wengi wangependa mrithi wa Papa Benedikti wa XVI awe kijana.
Wengi wangependa mrithi wa Papa Benedikti wa XVI awe kijana.Picha: VINCENZO PINTO/AFP/Getty Images

Rainer Maria Woelki ambaye ni mwenzake Meisner kutoka Berlin anasema hakuna kosa ikiwa papa mpya atakua kati ya miaka 60 na 70. Askofu huyo mkuu wa mji mkuu wa Ujerumani mwenyewe ana umri wa miaka 56 mmoja kati ya wale walio vijana katika jopo la makardinali. Aprili 2005, jopo hilo lilimchagua Kardinali Ratsinger kwa papa, siku tatu kabla ya kuadhimisha miaka 78 tangu kuzaliwa.

Nafasi ya Ulaya

Papa atatokea tena Ulaya au bara lingine ikiwa na maana kwa mara ya kwanza kuwa na Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani kutoka Afrika, Asia au Amerika kusini ? Pia jee atatokana na kundi la waliobobea kwa elimu na mwenye kuzungumza lugha kadhaa. Bila shaka hilo linaweza kuwa na msisimko wa aina yake.

Kundi la Wataliani katika jopo hilo la viongozi 150 wa Kanisa ni lenye nguvu likiwa na wajumbe 28 na huenda likaungana na wahafidhina kutoka Uhispania na Ufaransa. Hata hivyo kuchaguliwa kwa Mtaliani si jambo la uhakika kwa sababu Maaskofu nchini humo wamegawika katika makundi kadhaa.

Majina kutoka Amerika Kusini na Afrika

Kutoka Amerika kaskazini na hasa Marekani si jambo linalotarajiwa hata kidogo. Lakini majina yanayogonga vichwa vya habari kutoka Amerika kusini ni pamoja na Askofu mkuu wa Sao Paulo Odilo Pedro Scherer mwenye umri wa miaka 63 ambaye aliwahi kufanya kazi Vatikani kwa miaka mingi. Nchi yake ni moja wapo ya zile muhimu miongoni mwa Wakatoliki. Mwengine ni Ruben Salazar Gomez kutoka Colombia mwenye umri wa miaka 70.

Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson kutoka Ghana ni miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kuwa Papa.
Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson kutoka Ghana ni miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kuwa Papa.Picha: picture-alliance/dpa

Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson ndiye mgombea pekee muhimu kutoka bara la Afrika. Akiwa rais wa baraza la haki na amani la Kanisa Katoliki ni mtu anayesifika panapohusika na kushughulikia maamuzi magumu. Anazungumza lugha kadhaa na kuwa kivutio mpaka kwa Wajerumani.

Huenda kwa sasa, wakati jopo hilo likianza kukutana kesho, hakuna aliyetokeza kuwa na nafasi ya kushinda moja kwa moja. Lakini Wakati Benedikti wa XVI amejiuzulu kuwa Papa ,kuna usemi wa Kirumi usemao "Entrare Papa et Uscire Cardinale," Anaiyengia kuwa Papa hutoka akiwa tena Kardinali."

Mwandishi: Strack Christoph
Tafsiri: Mohamed Abdulrahman
Mhariri: Mohammed Khelef