NAJAF:Moqtada awapongeza wanamgambo wake kwa aliyouita ushindi | Habari za Ulimwengu | DW | 21.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAJAF:Moqtada awapongeza wanamgambo wake kwa aliyouita ushindi

Kiongozi wa kundi la washia wenye siasa kali nchini Iraq, Moqtada al Sadr amewapongeza wafuasi wake kwa kuwafanya wanajeshi wa Uin gereza kujiondoa katika mji wa Basra.

Jeshi la Uingereza linatarajiwa kuondoka katika kambi yao ya mwisho huko Basra na kwenda katika kambi ya jeshi la anga nje kidogo ya mji huo wiki chache zijazo.

Lakini makamanda wa Uingereza wamesisitiza kuwa kujiondoa huko si kwa kulazimishwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya makombora ya wanamgambo hao, na kwamba wataukabidhi mji huo kwa jeshi la Iraq.

Hata hivyo Moqtada a la-Sadr katika taarifa yake amesema kuwa hatua hiyo ni ushindi kwa wanamgambo wake na akatoa wito kwa wairaq kuungana kuyaondoa majeshi yote ya kigeni nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com