1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Wahamiaji 66 wazama wakijaribu kuingia Yemen kutoka Somalia

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DG

Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu 66 wamezama wakijaribu kuvuka bahari kutoka Somalia kuingia Yemen.

Watu 244 wengi wakiwa ni wasomali na waethiopia walikuwa wakisafiri kwa meli iliyokuwa imejaa kupita kiasi wakati wafanyibiashara ya magendo ya kuwasafirisha watu walipoanza kuwapiga baadhi yao na kuwalazimisha kuruka kwenye bahari ya Ghuba.

Msemaji wa shirika la wakimbizi la UNHCR amefahamisha kwamba kwa muda mrefu watu wamekuwa wakijazwa na kusafirishwa katika viboti vidogo na kusababisha hatari kubwa huku wasafirishaji hao haramu wakiwabughuthi wakimbizi.

Kiasi cha wahamiaji 439 wamekufa wakijaribu kuvuka bahari ya Ghuba ya Aden mwaka huu na wengine wapatao 500 wametoweka.